Diddy kizimbani, wanawe washindwa kuvumilia ushahidi uliotolewa

Diddy kizimbani, wanawe washindwa kuvumilia ushahidi uliotolewa

Kesi inayomkabili rapa kutoka Marekani, Sean “Diddy” Combs imesikilizwa jana Mei 12,2025 huku waendesha mashtaka wakiwaita mashahidi wawili, akiwemo afisa wa polisi pamoja na mwanaume aliyewahi kushuhudia Combs akimpiga Cassie.

Mapema jana kesi hiyo ilisikilizwa katika mahakama iliyopo jijini New York ambapo mwanamuzuiki huyo ameshitakiwa kwa makosa matano yakiwemo njama ya kufanya uhalifu (racketeering conspiracy), usafirishaji wa binadamu kwa ajili ya ngono, na usafirishaji kwa ajili ya uasherati.

Mashahidi wawili wa kwanza kutoa ushahidi

Katika kesi hiyo mashahidi wawili walitoa ushahidi wao ambapo Afisa wa Polisi wa Los Angeles alieleza jinsi alivyopokea simu ya dharura mwaka 2016 kutoka kwa Cassie Ventura kuhusiana na tukio la mashambulizi.

Ikumbukwe mwishoni mwa mwaka jana ilisambaa video ya Diddy ikimuonesha akimpiga aliyekuwa mpenzi wake Cassie tukio ambalo lilitokea kwenye moja ya hoteli iliyopo jijini New York.

Hata hivyo shahidi mwengine ambaye ni dansa wa kiume aitwaye Daniel Phillip aliweka wazi kuwa alilipwa maelfu ya dola ili kufanya mapenzi na aliyekuwa mpenzi wa Diddy, Cassie huku Combs akiwatazama na kuwaelekeza namna ya kufanya kitendo hicho.

Aidha dansa huyo aliweka wazi kuwa wakati wanafanya kitendo hiyo walitumia mafuta ya watoto huku Diddy akilalamika mafuta kuwa madogo. Mbali na hilo alishuhudia Combs akimpiga Cassie.

Ikumbukwe mwishoni mwa 2024 mafuta ya watoto yalizua gumzo katika mitandao ya kijamii baada ya zaidi ya chupa 1000 kukutwa nyumbani kwa Diddy wakati wa msako wa polisi.

Mabinti wa Diddy kuondoka wakati shahidi wapili akitoa ushahidi

Wakati wa kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa huku akipanda kizimbani shahidi wa pili ambaye ni Daniel watoto watatu wa kike wa Diddy walichukua uamuzi mgumu wa kuondoka Mahakani kutokana na kutoweza kuvumilia kusikiliza ushahidi aliokuwa akiuto mwanaume huyo aliyedai kulazimishwa kufanya ngono na Cassie.



Mabinti hao ambao ni Chance Combs, aliyemaliza shule ya Sekondari hivi karibuni na mapacha wenye umri wa miaka 18 D’Lila na Jessie waliondoka mahakamani mara mbili wakati Dainiel alipokuwa akitoa ushahid wa kumdharirisha baba yao.

Aidha Combs amekana mashitaka yote na iwapo atapatikana na hatia kwa makosa yote aweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela. Kesi hiyo inatarajia kuendelea leo Mei 13,2025 huku mashahidi wengine wakitoa ushahidi wao.

Baada ya watu kadhaa kumfungulia mashitaka mwanamuziki huyo, Machi 2024 mawakala za Usalama wa Ndani walifanya uchunguzi kwenye nyumba za Diddy ya Miami na Los Angeles wakichunguza tuhuma zinazomkabili za kujihusisha kwenye biashara za ngono na madawa ya kulevya.

Wakati wa uchunguzi huo moja ya vitu vilivyopatikana ni pamoja na mafuta ya watoto, vilainishi 1000 pamoja na dawa za kulevya jambo ambalo lilifanya Combs kukamatwa na polisi.

Septemba 16,2024 jijini New York , Diddy, alikamatwa na maafisa wa Idara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (Homeland Security Investigations).






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags