Watu 17 nchini Libya wahukumiwa kifo kwa kujiunga na kundi la IS

Watu 17 nchini Libya wahukumiwa kifo kwa kujiunga na kundi la IS

Mahakama nchini Libya imewahukumu kifo watu 17 baada ya kuwakuta na hatia ya kujiunga na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu (IS) na kufanya uasi kwa kutumia jina hilo, hii ikiwa ni kulingana na mwendesha mashitaka.

Aidha, mahakama hiyo imewahukumu watu wawili kifungo cha maisha jela na wengine 14 vifungo vya muda mfupi.

Kwa pamoja washukiwa hao walikutwa na makosa ya kujihusisha na vitendo vingine vyenye mafungamano na kundi hilo la IS, mashambulizi dhidi ya amani ya taifa na jamii pamoja uhalifu wa kutumia silaha, katika mji wa Sabratha na viunga vyake magharibi mwa taifa hilo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags