Watu 12 wafariki dunia huku  zaidi ya 50 wamejeruhiwa

Watu 12 wafariki dunia huku zaidi ya 50 wamejeruhiwa

Watu 12 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la abiria la kampuni ya Frester lililokuwa likitoka Bukoba kwenda Dar es Salaam kugongana uso kwa uso na Lori lenye shehena ya saruji.

Ajali hiyo ambayo imetokea saa sita usiku wa kuamkia leo Februari 9, 2023 katika Kijiji Cha Silwa Pandambili barabara kuu ya Dodoma - Morogoro huku chanzo cha ajali hiyo ikidaiwa ni dereva wa basi kutaka kulipita gari lililokuwa mbele yake bila kuchukua tahadhari

Hata hivyo Mkuu wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Awadh Haji amefika eneo la ajali na kutoa rai kwa madereva kuzingatia usalama na sheria za barabarani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags