Vyakula vinavyoimarisha afya ya ngozi

Vyakula vinavyoimarisha afya ya ngozi

Hellow, its another day, kama kawaida yetu kupitia kipengele chetu pendwa kabisaa cha Fashion ili kuweza kujua mambo kadha wa kadha yanayohusu upande wa urembo bwana.

Leo tutaangazia vyakula vinavyoimarisha afya ya ngozi, kama unavyofahamu mwanamke bila urembo bado haujakamilika bwana au nadanganya?

Yes, iko hivyo ili uweze kuwa mrembo na bora Zzidi lazima ujipende na ufuatilie ngozi yako ujue unailea vipi bwana, ungana nami kwenye dondoo hii fupi ili uweze kupata maarifa zaidi kwenye masuala haya.

Bila kupoteza, tuanze moja kwa moja kwa kuangalia ni vyakula gani ambavyo vinaweza kuimarisha afya ya ngozi karibu.

 

ASALI

 

Asali ambayo hutengenezwa na nyuki huwa na viambato asilia na ni moja ya chakula muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya ya ngozi. Asali husaidia kutunza na kuhifadhi unyevu kwenye ngozi na ina kiwango kikubwa cha sukari na asidi ambazo huzuia vijidudu wanaozaliana kwenye ngozi.

Tumia asali kwa kupaka wakati wa kuoga, kisha acha kwa muda na ioshe. Kufanya hivyo husaidia kuinawirisha ngozi. 

MAYAI

Mayai pia ni muhimu kwa afya ya ngozi yako, kiini cha yai huwa na vitamini A na B, huku sehemu yenye ute ikiwa na protini nyingi ambayo ni muhimu pia kwa Ngozi. Ute wa yai ni muhimu katika kuifanya ngozi kuwa nyororo na yenye kung'aa na pia husaidia ngozi kujilinda vizuri na mionzi ya jua.

MATUNDA

Matunda nayo ni muhimu pia hususani chungwa na limao ambayo husaidia kuimarisha afya ya ngozi, kwa sababu husaida kutengeneza collagen ambayo ni aina ya protini inayotengeneza ngozi.  

Ndani ya matunda hayo huwa na Vitamini C, ambayo husaidia sana kuondoa uvimbe na mikunjo ya ngozi na hivyo kuilinda ngozi isizeeke mapema.

 

MBOGA ZA MAJANI

Mboga za majani pia ni muhimu kwa afya ya ngozi kama tujuavyo zimesheheni vitamin na virutubisho vya aina mbalimbali vyenye faida kubwa kwa ngozi na mwili kwa ujumla. Mboga hizi za majani husaidia ngozi kuzalisha seli mpya na kuondoa zile zilizokufa, hivyo kupunguza ukavu na kutunza ngozi na kuifanya ing’are na kuvutia. 

VYAKULA VYA BAHARINI

Vyakula vya baharini kwa ujumla ni vizuri kwa afya ya ngozi. Vyakula vingi vya baharini vina kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi. Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi, kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi na husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi.

Aloooooh, unaweza kusema wow kwa lugha ya kigeni bwana, kwanini ukae na ngozi ambayo haina mvuto na mambo ya asili ni kama haya? 

Nikwambie tu waswahili wanasema ukitaka uzuri uzurike bwana.

Basi ni wakati wako wa kuweka mazingira mazuri ukiwa kama mwanamke au binti unayependa urembo wa asili nikusihi tu usikose kufuatilia jarida la Mwananchi Scoop ili uweze kupata taarifa nyingi zaidi.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags