Namna Ya Kutengeneza Halwa

Namna Ya Kutengeneza Halwa

Halwa ni aina ya kitafunwa kitamu, laini na cha kupendeza ambacho hupatikana katika maeneo mbalimbali duniani, hususan Asia ya Kusini, Mashariki ya Kati, Afrika ya Kaskazini, na Afrika Mashariki (hasa Pwani kama Zanzibar, Mombasa, Tanga n.k).

 

Halwa huchukuliwa kama dessert au kitafunwa cha heshima kinachotolewa katika sherehe, misiba, mikusanyiko ya kifamilia, na hata mwezi mtukufu wa Ramadhani. Neno Halwa linatokana na neno la Kiarabu ambalo linamaana ‘Tamu’.

 

Mbali na kuwa kitafunwa kitamu lakini kwenye baadhi ya maeneo kimekuwa adimu kutokana na watu wake kutojua kutengeneza kitafunwa hicho. Ungana nasi kujua dondoo ya kutengeneza Halwa mwanzo mwisho.

 

MAHITAJI

  1. Unga wa muhogo nusu
  2. Sukari – 1 ½ kikombe
  3. Maji – 2 ½ kikombe
  4. Samli au siagi ½ kikombe (unaweza kuongeza kama ukitaka iwe laini sana)
  5. Hiriki ya unga – 2 kijiko cha chai
  6. Rangi ya chakula kiasi
  7. Karanga, Korosho au Ufuta (sasa utachagua kimoja kati ya hivyo vitatu)
  8. Majani ya chai kijiko kimoja (Siyo lazima weka kama unataka halwa yako iwe nyeusi sana)
  9. Chumvi kidogo

 

NAMNA YA KUPIKA

 

  • Chukua bakuli weka maji pamoja na unga wa muhogo kisha koroga mpaka uchanganyike kabisa na uweke pembeni.
  • Baada ya hapo chukua rangi yako ichanganye na maji kiasi kisha nayo uweke pembeni.
  • Baada ya kufanya hayo chukua sufuria yako bandika jikoni weka maji vikombe viwili, majani ya chai, sukari, rangi uliyokoroga, hiriki na chimvi kidogo, kisha koroga mpaka pale sukari itakapochanganyika na maji kabisa.
  • Mchanganyiko wako ushaanza kuchemka chukua unga wa muhogo ambao umekoroga na maji kisha umimine jikoni kwenye sufuria yako na uanze kukoroga.
  • Utakapokuwa unakoroga hautakiwi kuachia yaani unakoroga moja kwa moja, ukishakuwa mzito utaanza kusonga mpaka pale utakapobadilika rangi ya Brown kwa dakika 15.
  • Baada ya kuona Halwa yako imeshakuwa ya Brown utaanza kuweka siagi yako vijiko vitatu , halafu utaendelea kusongo utafanya hivyo mpaka pale siagi yako uliyopima uimalize na ili uone halwa yako imeiva utaanza kuona inavutika.
  • Na baada ya hapo utaepua kisha umwagie karanga, korosho au ufuta ukipenda na mpaka hapo Halwa yako itakuwa tayari kwa ajili ya kula.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags