Kuvaa stara ni mtindo wa mavazi unaoendana na heshima, maadili na utu. Kuvaa stara siyo tu suala la muonekano wa nje, bali pia ni njia ya kutoa mfano mzuri kwa wengine na kuonesha kiwango cha kujiheshimu.
Kwa miaka ya hivi karibuni kuvaa stara imekuwa kwa kiasi kikubwa kwani hapo awali mavazi ya stara yalipendelewa kuvaliwa haswa na watu wa dini ya Kiisalamu, lakini kwasasa mavazi hayo hususani Abaya yamekuwa yakivaliwa na watu wa dini mbalimbali na hii ni kutokana na mavazi hayo kuwafanya watu kuwa na stara.
Faida za kuvaa mavazi ya stara
- Kujiheshimu na kuheshimika
Moja ya faida kubwa ya kuvaa stara ni kujiheshimu na pia kuheshimiwa. Unapoamua kuvaa mavazi ya stara, unatoa taswira ya heshima ambayo huwafanya watu wakuchukulie kwa uzito. Hata kama kuna watu waliokuwa na mawazo mabaya juu yako, mavazi yako ya heshima yanaweza kubadili mtazamo wao na kukuona kwa heshima zaidi.
- Kuhimili kila mazingira
Mtu anayevaa stara anaweza kuingia sehemu yoyote rasmi iwe kazini, kanisani, msikitini au kwenye mikutano bila kuwa na wasiwasi wa kukataliwa au kusemwa.
- Kulinda mwili na hadhi yako
Katika mitandao ya kijamii baadhi ya wanawake wamekuwa wakiangaika na vitu vya kutumia ili waweze kuwa na joto, hivyo basi siri nyingine na kuibia kuwa mavazi ya stara pia husaidia kulinda mwili wako kwa kuupa joto, lakini pia hulinda utu na hadhi yako.
- Kuwa mfano mzuri kwa jamii
Kwa kuvaa stara, si tuu kwa ajili ya kukuletea heshima au kujiheshimu bali pia mavazi hayo yanamfanya mtu kuwa mfano wa kuigwa hasa kwa vijana na watoto ambapo jambo hilo litasaidia kujenga jamii yenye maadili na nidhamu ya mavazi.
- Kuepusha usumbufu wa kijamii
Mavazi ya stara husaidia kuepusha maneno ya kejeli, mitazamo ya kiholela, au usumbufu kutoka kwa watu wasiokuwa na nia njema. Unapovaa kwa heshima, unajikinga na hali zisizofaa zinazoweza kukupunguzia amani au staha yako.
Leave a Reply