Kim Atoa Ushahidi Kesi Ya Ujambazi, Asema Alidhani Atakufa

Kim Atoa Ushahidi Kesi Ya Ujambazi, Asema Alidhani Atakufa

Nyota wa vipindi vya Televisheni na mjasiriamali, Kim Kardashian leo Jumanne Mei 13, 2025 ameiambia mahakama ya Paris nchini Ufaransa kwamba alidhani angenyanyaswa kimwili na kuuawa baada ya kuvamiwa na majamabazi akiwa Hotelini nchini humo wakati wa wiki ya mitindo 'Paris Fashion Week' mwaka 2016.

Akizungumza mahakamani hapo wakati wa kutoa ushahidi Kim amesema katika tukio hilo alivamiwa na watu 10 na kuibiwa vito vyenye thamani zaidi ya dola 9 milioni sawa na sh 26 bilioni.

Hii inakuwa mara ya kwanza kwa Kim kuhudhuria mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo ambapo waharifu walikuwa wamevaa kama maafisa wa polisi na kumnyooshea bunduki, na kumfunga kamba kisha Kumfungia bafuni na baada ya kukamilisha zoezi lao la wizi walitoweka eneo la tukio.

Baada ya washukiwa kufikishwa mahakamani wakiwa ni wanaume tisa na mwanamke mmoja wamepewa jina la Majambazi Wazee 'Grandpa Robbers' kwani baadhi yao wana umri wa miaka kati ya 60 hadi 70 na wanakabiliwa na mashtaka ya unyang'anyi wa kutumia silaha kuiba wakiwa na genge lao.

Utakumbuka, mmoja kati ya wadaiwa wa wizi wa vito vya thamani vya Kim Kardashian aliripotiwa kufariki dunia ghafla kabla ya kuanza kusikilizwa kesi kesi hiyo Jumatatu Mei 5, 2025.

Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na TMZ zinasema mtuhumiwa huyo aliyefahamika kwa jina la ‘Marceau Baum-Gertner’ alifariki dunia Machi 6 mwaka huu Paris, Ufaransa huku sababu ya kifo chake haijajulikana.

Merceau anaekisiwa kuwa na umri wa miaka 35-78 alitarajiwa kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu ya Mei 5, 2025, pamoja na kundi lake kwa madai ya kuhusika na wizi wa zaidi ya dola milioni 10.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags