Tanzania na Kenya kuendeleza ushirikiano katika sekta ya gesi na umeme

Tanzania na Kenya kuendeleza ushirikiano katika sekta ya gesi na umeme

Waziri wa Nishati nchini, January Makamba pamoja na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Isaac Njenga wamekutana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Kenya katika Sekta ya Umeme na Gesi.

Makamba amemueleza Balozi Njenga kuwa Tanzania ipo tayari kuendeleza ushirikiano na Kenya katika Sekta ya Gesi na Umeme kwani nchi hizo tayari zina ushirikiano kwenye sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu ya barabara na anga.

Kuhusu mradi wa usafirishaji Gesi kutoka Tanzania kwenda Kenya, amesema mradi huo ni wa kipaumbele kwa viongozi wakuu wa nchi hizo mbili na tayari timu za majadiliano kutoka Kenya na Tanzania zimeshaundwa na zinaendelea na kazi ya uandaaji wa nyaraka zitakazowezesha mradi huo kusonga.

Aidha Balozi Njenga ameeleza kuhusu utayari wa Kenya katika kutekeleza makubaliano ya ushirikiano yaliyoingiwa kwenye mradi wa usafirishaji gesi kutoka Tanzania na miradi ya usafirishaji wa umeme kwa msongo wa KV 400 ambayo itawezesha nchi hizi mbili kuweza kuuziana umeme.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post