Tajiri Murdoch atarajia kufunga ndoa kwa mara ya tano

Tajiri Murdoch atarajia kufunga ndoa kwa mara ya tano

Tajiri wa vyombo vya habari kutoka nchini Australia Rupert Murdoch, mwenye umri wa miaka 92, ametangaza kuchumbiana na mpenzi wake Ann Lesley Smith 66, kasisi wa zamani wa polisi.

Wawili hao kwa mara ya kwanza walikutana mnamo Septemba, katika hafla kwenye shamba lake la mizabibu, huko mjini California.

Mfanyabiashara huyo alifunguka katika gazeti lake la New York Post, na kueleza kuwa, “Niliogopa kuingia kwenye mapenzi lakini nilijua hii ingekuwa ya mwisho kwangu na iwe hivyo kwa sababu nina furaha,” alisema Murdoch.

Tajiri huyo aliachana na mke wa nne Jerry Hall mwaka jana, na mwanamama Ann yeye akiwa ni mjane.

Mfanyabiashara huyo alieleza kuwa harusi itafanyika mwishoni mwa majira ya joto na wanandoa watatumia muda wao wa mapumziko (Honeymoon) California, Montana, New York na Uingereza.

Ikumbukwe tu tajiri hiyo hapo awali aliwaoa wanawake hawa: Mhudumu wa ndege kutoka Australia Patricia Booker, mwandishi wa habari mzaliwa wa Scotland Anna Mann, mjasiriamali mzaliwa wa China Wendi Deng, na Jerry Hall.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags