Serikali yatoa utafiti vijana wasio na ajira nchini

Serikali yatoa utafiti vijana wasio na ajira nchini

Serikali imesema Utafiti wa Watu wenye uwezo wa kufanya Kazi wa Mwaka 2021 unaonesha Vijana wenye umri wa Miaka 15 hadi 35 ambao wana Ukosefu wa ajira ni 1,732,509 sawa na 12% ya nguvu Kazi ya Vijana wenye umri huo

Aidha akijibu swali Bungni  Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Patrobas Paschal Katambi amesema

“Katika kuhakikisha vijana wanaendelezwa ili kushindana katika soko la ajira ndani na Nje ya Nchi, Serikali imeweka mkakati wa Kitaifa wa kukuza ujuzi wa Miaka 10 ambapo imefanya Maboresho ya Mitaala ya Elimu ya juu na ya kati kwa mafunzo ya Stadi ya Ufundi.”

Ebwana eeeh!! Unaweza kudondosha comment yako hapo chini na kutoa maoni yako juu ya suala hili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags