Raisi Samia: Vijana acheni kunywa supu ya pweza

Raisi Samia: Vijana acheni kunywa supu ya pweza

Wataalamu wa afya wanashauri watu kufanya mazoezi ili kuimarisha afya ya mwili lakini hii kwa vijana imekuwa tofauti wengi hutumia muda wao kushinda gym kwa kufanya mazoezi ili kupata muonekano mpya kama kuongeza hips, kupunguza uzito, kuwa na kifua kipana wenyewe wanaita “six packs’’ na kupuuzia swala la mlo kamili.

Basi bhana mama leo kaamua kulitolea uvivu na kukemea suala la vijana kutokula mlo kamili ili kwenda na wakati kwa kuwa na muonekano fulani. Rais Samia ameyasema hayo katika  hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji wa shughuli za lishe leo Septemba 30, 2022, jijini Dodoma.

Pia amewataka vijana kula mlo kamili ili kusaidia uzalishaji mzuri ndani ya jamii katika uchumi na kuzaliana ili kuongeza rasilimali watu na sio kunywa supu ya pweza pekee kama vijana wanavyodhani.

"Kwanini watoto wetu wakifika wakati wa kuongeza jamii wanahangaika, mara supu ya pweza. Tuna tatizo na mnalijua, mnalificha watafiti fanyeni utafiti tujue kama hili suala liko nje ya lishe bora,” Rais Samia alisema.

 

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags