JE WAJUA:  Watu wanaoishi China ni zaidi ya watu Afrika nzima

JE WAJUA: Watu wanaoishi China ni zaidi ya watu Afrika nzima

Kali nyingine hii hapa!

Pengine ulikuwa unajua kuwa nchi ya China inaongoza kwa watu wengi duniani, lakini je ulijua kuwa uwingi huo wa watu ni sawa na watu wa bara zima la Africa?

Ripoti kutoka Umoja wa Mataifa inasema kuwa uwingi wa watu duniani utafika bilioni 8 mnamo November, 2022, huku China ikiwa inaongoza kwa watu wengi, ikiwa na watu sawa asilimia 19 ya watu wote duniani.


China inaongoza kwa uwingi wa watu ikiwa na watu Bilioni 1.44, ikifuatiwa na India yenye watu Bilioni 1.39, sawa na asilimia 19 na 18, according to World Population Prospects 2019, wakati huohuo, Afrika ina asilimia 17 tu za watu wote duniani.

Hata hivyo, huwenda nchi ya India ikaipita nchi hiyo ya China kwa kuongezeka kwa watu nchini humo mara dufu, ambapo ripoti zinaonesha kuwa hadi kufika mwakani, nchi ya India itakuwa na watu zaidi ya nchi ya China, huku China ikitabirikiwa kupunguzika kwa watu takriban Milioni 31.4 kati ya mwaka 2019 na 2050.



Kwasasa, bara la Asia linashikilia namba ya kwanza kwa kuwa na watu wengi, ikiwa na jumla ya watu bilioni 4.7, sawa na asilimia 61 ya watu duniani, ikifuatiwa na Afrika ikiwa na watu bilioni 1.3, sawa na asilimia 17, Europe na watu Milioni 750, sawa na asilimia 10, Latin America na the Caribbean na watu Milioni 650, sawa na asilimia 8, America Kaskazini na watu Milioni 370, sawa na asilimia 5 na Oceania ikiwa na watu Milioni 43.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags