Harmonize: Ndoto yangu kuwa na familia yenye furaha

Harmonize: Ndoto yangu kuwa na familia yenye furaha

Ebwana niaje mwanagu wa faida? Furaha ni kitu pouwa sana katika maisha ya mtu yoyote na ukiwa na furaha unaweza kufikiria vizuri. Basi bhana Mmakonde amefunguka kupitia Instastory yake kuwa moja ya ndoto yake ni kuwa na familia yenye furaha.

Msanii huyo miezi kadhaa iliyopita alikuwa na ugomvi mzito kati ya mpenzi wake Kajala na mtoto wake Paula na kusababisha uadui baina yao ,kuomba msamaha kwa mtu uliyemkosea sio dhambi wala udhaifu mmakonde aliamini hilo na kuamua kumuomba msamaha mpenzi wake na kurudisha malavidavi upya.

Kupitia Instastory ya Harmonize amepost video ikimuonyesha kajala na paula wakiwa na furaha na ujumbe ukisema, "Ilikuwa ni ndoto kuona familia yangu inafuraha tena. Mungu amelifanikisha hilo. Hii video inanifanya nijihisi mwanaume wa kweli, kila alichopanga Mungu kitatokea pia usikate tamaa!”

Dondosha comment yako hapo chini, unafanya nini ili kuwa na furaha muda wote?






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags