Watatu hatiani kwa mauaji ya  rapper XXXTentacion

Watatu hatiani kwa mauaji ya rapper XXXTentacion

Mahakama kutoka nchini Marekani imewakuta na hatia ya mauaji ya daraja la kwanza na wizi wa kutumia silaha Dedrick Williams mwenye umri wa miaka (26), Trayvon Newsom (24) na Michael Boatwright (27) baada ya ushahidi kuthibitisha ushiriki wao katika mauaji ya rapper, Jahseh Onforoy, maarufu kama XxxTentacion, mwaka 2018.

XXXTentacion ambae alikuwa na umri wa miaka 20 aliuwawa huko Deerfied Beach, Florida, baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi na watu hao walichukua begi lililokuwa na dola za Marekani 50,000, Takriban Milioni 117 za Kitanzania.

Aidha, hukumu imepangwa kutolewa Aprili 6, 2023 na huenda watatu hao wakafungwa kifungo cha maisha.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags