Wanafunzi 8 wafariki katika ajali ya boti nchini Ghana

Wanafunzi 8 wafariki katika ajali ya boti nchini Ghana

Mamlaka nchini Ghana inachunguza hali iliyosababisha kuzama kwa boti iliyouwa watoto nane wa shule kwenye ziwa Volta, katika eneo la kusini mashariki.

Mamlaka za eneo hilo zilisema watoto wengine 12, waliokuwa ndani ya boti hiyo iliyopinduka siku ya Jumanne walinusurika.

Watoto hao walikuwa wakisafiri kutoka kijiji cha wavuvi cha Atikagome kwenda kwa jamii ya Wayokope ambapo ndipo shule yao ilipo.

Miili ya watoto wavulana watano na wasichana watatu wenye umri wa kati ya miaka 5 na 12 waliofariki imetolewa, Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Majanga la Ghana lilisema.

Tukio hilo limeibua wito kwa serikali kuboresha miundombinu ya usafiri katika maeneo ya vijijini.

Ajali za boti hutokea mara kwa mara kwenye ziwa Volta kwa kiasi fulani kutokana na kujaa kupita kiasi, boti zilizojengwa vibaya na kuwepo kwa vishina vya miti majini.

Mnamo Aprili mwaka jana, watu saba walifariki katika ajali kama hiyo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post