Sifa za kuwa nazo ili kupass interview za kazi

Sifa za kuwa nazo ili kupass interview za kazi

 

So you are about to hit that interview, you are nervous and you don't know what to do? Hii ndio sababu nipo kwaajili yako. Take a breath, relax na usome tips za kukusaidia uonekane upo vizuri. Ukipitia haya mambo anayosema dada Detty, hakika you will blow the mind of your interviewers! Lets GO!


       
1. Vaa Nadhifu

Hakikisha kuwa siku hiyo umevaa vizuri, hasa kutokana na kazi unayoipigania. Mara nyingi hushauriwa kuvaa kiasi, sio Sanaa na sio kidogo. Unaweza vaa suti, au shati na suruali/sketi, ama gauni na koti, na ukachomekea. Kumbuka, kuna mengi yataangaliwa kwa siku ya kwanza.

 

  1. Jua jinsi ya kujielezea

Kujielezea ni muhimu mno, kwani ukikosea tu kitu kimoja, UMEFELI! Hakikisha unajua kuelezea historia yako, hasa ile ya kazi. Kuelezea matarajio yako, Pamoja na uwezo uliokuwa nao ambao utakuwa wa manufaa pale ambapo unataka kupata kazi.

 

  1. Jiandae kwa kuijua kampuni kiundani

Kabla ya kwenda kwenye interview yeyote ile, fanya uchunguzi juu ya hiyo kampuni, uongozi uliopo, ndoto za kampuni, Pamoja na malengo. Hii itakusaidia kujua ni namna gani utaweza kujielezea, na kuonesha kuwa utahitajika katika tufikia malengo hayo.

 

  1. Waoneshe thamani

Kila kampuni ina hitaji kuajiri mtu ambae ataweza kuongeza thamani katika biashara yao, hivyo ni muhimu sana kuonesha thamani yako katika kampuni, endapo watakuchagua. Hakikisha unajua wanahitaji mtu mwenye maarifa ya aina gani, ikiwezekana, uwe na Ushahidi wa vitu ulivyovifanya ambavyo vinaweza kuonesha uwezo wako. Kama hauna hivi, nakushauri uanze kujipanga kuwa navyo.

 

  1. Fanya kila kitu kuwa kuhusu wao na sio wewe

Waajiri hujali kampuni yao na maendeleo yake tu, na si vinginevyo!  Hata kama una ujuzi kwa kiasi gani, usifanye mahojiano hayo yakawa kuhusu wewe na namna gani uko vizuri sana, kwani unaweza kuonekana unajikweza! Ili kujiongezea nafasi ya kupata nafasi hiyo ya kazi, hakikisha unajibu kila swali kulingana na wao, ili waweze kuona kuwa wewe unahitaji hiyo kazi kwaajili ya kuiendeleza kampuni, na si vinginevyo!

 

Ukizingatia machache haya, hakika utajiongezea nafasi ya kuchaguliwa katika nafasi za kazi. Nakutakia kheri katika safari hii ya utafutaji kazi, JIAMINI, UNAWEZA!






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Detricia Pamba

A Digital Journalist, Content Creation Executive at Mwananchi Communications Ltd and Chief Editor of Mwananchi Scoop. I'm also writes stories around Technology, every Wednesday on Mwananchi Scoop. My other famous segments on Mwananchi Scoop include LISTI and WHO’S HOT.


Latest Post

Latest Tags