Mwaka unakata msanii wa Marioo kimya!

Mwaka unakata msanii wa Marioo kimya!

Ukiwa unakaribia kumalizika mwaka mzima msaa wa Marioo, Stans 'Mr Vest' bado hajaonyesha makali ambayo mashabiki walikuwa wanategemea kutoka kwake.

Staa huyo alitambulishwa Agosti 29, 2024, ambapo alipokelewa vizuri, lakini hadi sasa hakuna makali yoyote ambayo amefanikiwa kuyaonyesha.

Tangu msanii huyo atambulishwe kwenye lebo hiyo mwaka uliopita amewahi kusikika kwenye projekti moja pekee iitwayo '2025', aliyoshirikishwa na Marioo. Kazi hiyo ilitoka rasmi Agosti 30, 2024, ambayo pia inapatikana kwenye Albamu yake ya The Godson.

Mapokezi ya msanii huyo tangu kutambulishwa kwake yalikuwa makubwa na mashabiki wengi walipenda uwezo wake kwenye '2025'. Ambapo pia alifanikiwa kuteka kiu ya mashabiki wengi kutamani kumsikia tena na tena. Lakini hajawa hiyo, mpaka leo Agosti 18, 2025, msanii huyo amebakisha siku 11 atimize mwaka tangu asainiwe kwenye lebo ya Bad Nation akiwa hana kazi yoyote mkononi.

Hii ni hali ya utofauti kama ilivyozoeleka kwenye lebo nyingine kubwa duniani pindi msanii anapotambulishwa. Akiwa na moto wake uleule huachia projekti kubwa inaweza kuwa Ep kwa maana ya Extended Playlist au Albamu na kama hiyo itashindikana basi anaweza kuanza na ngoma mfululizo, ili kutambulisha saundi yake kwa mashabiki na kujiokotea wafuasi.

Hali hii inaanza kufanya niamini kauli ya msanii wa Hiphop nchini, Nyandu Tozi ambaye aliwa kusema "Ni ngumu msanii kumsimamia msanii kwenye kazi zake za muziki. Kwa sababu wote wana malengo sawa na wapo kwenye soko moja,"

Lakini nikirudi nyuma naona mbona kuna wasanii wameweza kuwainua na kusimamia wasanii wengine. Diamond Platnumz ameweza kuwainua Harmonize, Rayvanny, Lava Lava, Zuchu na sasa D- Voice



Wakati msanii wa Bongo Fleva, Zuchu anatambulishwa Wasafi Aprili 2020, aliachia Ep yake ya kwanza 'Iam Zuchu' usiku huohuo wa Aprili 12, 2020. Harmonize alitambulishwa Wasafi na ngoma yake ya Aiyola iliyotoka Novemba 6, 2015, Rayvanny alikuja na Kwetu iliyotoka Aprili 14, 2016,

Uvumilivu unahitajika kwenye maisha ya muziki lakini kuna vitu vinakatisha tamaa msanii kutambulishwa mwaka mzima bila kuachia ngoma yoyote. Muziki ni kazi kama kazi nyingine mfano utajisikiaje kupata mtaji na kuwekeza kwenye duka ambalo halijafunguliwa mwaka mzima licha ya kuwa na vitu ndani?

Ukimya wa Stans unawaumiza hata mashabiki wake. Siku tatu zilizopita msanii huyo alichapisha picha kwenye ukurasa wake wa Instagram asilimia kubwa ya maoni yaliyotolewa, mashabiki wanamtaka kuachia ngoma nyingine.

Wasiwasi wa mashabiki wengi kwa Stans ni kwamba yasije kumkuta kama yaliyomkuta mwanamuziki Hanstone ambaye inaelezwa alitakiwa kutambulishwa Wasafii kabla ya Zuchu lakini kutokana na kuwekwa benchi kwa muda mrefu aliamua kujiengua na baadaye kuonekana hana uvumilivu






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags