Alichofanya Dolly Parton Kwa Mchepuko Wa Mumewe

Alichofanya Dolly Parton Kwa Mchepuko Wa Mumewe

Marekani. Maisha ya baadhi ya mastaa hutawaliwa na kiki na trending ili majina yao yaendelea kutamba mjini. Lakini mbali na kutaka kuiteka mitandao ya kijamii yapo ambayo yanawasibu katika maisha yao halisi.

Hapa nakusogezea stori halisi kutoka kwa nyota wa muziki wa Country duniani, Dolly Parton, kuhusiana na wimbo wake maarufu wa “Jolene” ambao aliuaimba kwa ajili ya mchepuko wa mumewe.

Mwaka 1970 mwanamuziki Dolly alitamba kupitia wimbo huo, aliweka wazi kuwa aliuandika kwa ajili ya kumuomba mchepuko wa mume wake ambaye alikuwa akifanya kazi benki aachane naye kwani hakuwa na mwanaume mwingine zaidi yake.



“Kulikuwa na msichana mrembo sana, nywele nyekundu, macho ya kijani. Alifanya kazi benki na mume wangu Carl Dean alikuwa akiingia mara kwa mara. Nilijua kuna kitu kinaendelea kati ya watu hawa wawili nikasema nimuandikie wimbo.

“Sikuwahi kufikiria kwamba Carl angeniacha. Lakini kuna kitu kilinifanya nihisi kutishika. Nilihisi kuwa na hofu ya kumkosa. Ndio maana nikamwomba Jolene kwa sauti ya maumivu aniachie mpenzi wa maisha yangu,” alisema kwenye moja ya mahojiano yake

Aidha alifunguka kuhusu jina la wimbo ambapo alieleza kuwa alilipata kwa mmoja wa shabiki yake.

“Siku moja nilipokuwa nikisaini sahihi kwa mashabiki, msichana mdogo alinijia. Alikuwa na nywele nyekundu na macho ya kijani. Nilimuuliza jina lako nani? Akasema Jolene. Nikasema, hilo ni jina zuri sana, lazima nitumie kwenye wimbo wangu,” amesema 

Wakati wimbo huo unaachiwa ulifanikiwa kutamba katika chati mbalimbali za muziki ikiwemo nafasi ya kwanza kwenye Billboard Country Charts nchini Marekani, kuwa wimbo wa kwanza kwa Dolly kuingia kwenye Billboard Hot 100 huku ukinyakuwa tuzo mbalimbali ikiwemo ya heshima. 

Chakuvutia ni kwamba, pamoja na hofu ya kumpoteza mumewe, ndoa ya Dolly Parton ilikuwa imara hadi kifo kilipomkuta mumewe mapema mwaka huu. Huku wakiwa na zaidi ya miaka 50 kwenye ndoa .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags