Genghis Khan, alizaliwa Temüjin mwaka 1162 nchini Mongolia, alikuwa kiongozi shupavu wa kijeshi na mjenzi wa dola kubwa zaidi duniani. Akifariki dunia mwaka 1227, lakini sehemu alipozikwa bado ni siri kubwa hadi leo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mbalimbali vinadai kuwa watu wote ambapo walihudhuria katika mazishi yake wote waliuawa na kisha askari ambao walikuwa wakishirikiana na Khan na wao walijiua kwa kujinyonga ili kupoteza ushahidi wa kutoa taarifa za kaburi lilipo.
Aidha kufuatia na hilo Wanasayansi na wachambuzi wa mambo ya kihistoria wanajaribu kutumia teknolojia za kisasa kufanya uchunguzi kujua sehemu aliyozikwa mtu huyo lakini mpaka leo hii jitihada zao zimekonga mwamba kwani hakuna chochote walichokipata
Baadhi ya watu wanaamini kuwa kaburi hilo huwenda likawa katika milima ya Khangai au Khentii, huko Mongolia huku wengi wao wakifunguka kuwa kaburi hilo kuwa fumbo ni kwa lengo likiwa ni kutunza jina, heshima yake ili iwe sawa hata baada ya kifo chake

Leave a Reply