Blue Ivy Amewazidi Mastaa Kwa Tuzo

Blue Ivy Amewazidi Mastaa Kwa Tuzo

Waswahili wanasema mtoto wa nyoka ni nyoka na hili limejidhihirisha kwa mtoto wa mastaa Beyoncé na Jay-Z, Blue Ivy Carter ambaye ameonyesha ukubwa wake akiwa na umri wa miaka 13 tu ambapo amefanikiwa kunyakua tuzo ambazo hata watu wazima bado wanazitamani.

Safari yake ilianza akiwa mdogo wa siku mbili ambapo sauti yake ilisikika kwa mara ya kwanza kwenye wimbo wa baba yake uitwao ‘Glory’ na kuufanya wimbo huo kuingia kwenye chati za Billboard.


Lakini dunia ilimtambua zaidi baada ya kuonekana katika wimbo wa ‘Brown Skin Girl’ ambao aliimba pamoja na mama yake Beyonce, kupitia wimbo huo Blue alikusanya tuzo kama BET Award (2020), NAACP Image Award (2020), Soul Train Music Award (2020), pamoja na Grammy (2021).

Kupitia rekodi hiyo Blue aliandika historia ya kuwa msanii mdogo kabisa kupewa heshima hiyo ya Grammy ambapo kufuatia na hilo baadhi ya mashabiki wakatabili kuwa huwenda mtoto huyo akarithi mikoba ya mama yake.

Si tuzo hizo tu lakini pia Blue Ivy aliwahi kuchukua tuzo ya MTV VMA, tena akitajwa kuwa mshindi mdogo zaidi kwenye historia ya tuzo hizo, mbali na hizo hivi karibuni, ameibuka tena kidedea akiondoka na tuzo ya BET YoungStars Award kwa mara mbili mfululizo (2024 na 2025).

Mbali na kuonesha umahiri wake kwenye muziki lakini pia ameonesha kipaji chake katika uigizaji ambapo sauti yake imesikika katika katuni ya Mufasa: The Lion King (2024). Vile vile alifanikiwa kuonesha umahiri wake wa kudance katika ziara ya mama yake Renaissance World Tour.

Akiwa na miaka 13 pekee, Blue Ivy tayari ameshinda Grammy, BET, NAACP, Soul Train, VMA na kutambulika kimataifa kama kipaji kipya. Kwa jumla anahesabiwa kuwa na zaidi ya tuzo 10 kubwa mkononi mwake.

Kutokana na ukubwa huo Blue amewapiku mastaa kama Nicki Minaj, Snoop Dogg, Katy Perry, Tupac (marehemu), na Diana Ross ambao hawajawahi kushinda Grammy tangu waingie katika tasnia ya muziki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags