Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Guinness World Records’, ambao wamethibitisha ndio vazi lenye mikono mirefu zaidi wameweka wazi kuwa mikono hiyo inaurefu kuliko sanamu la Statue of Liberty pamoja na bwawa la Olimpiki.

Samuel fundi cherehani ambaye pia ni mwanafuzi katika chuo cha ‘Chukwuemeka Odumegwu Ojukwu University’ ameeleza kuwa hatua inayofuata sasa ni kulitembeza vazi hilo duniani kote ili watu waweze kuliona.
“Ninataka kulipeleka kwenye miji na nchi tofauti ili watu waone jinsi lilivyo,” alisema kwa furaha.
Alitengeneza vazi hilo ndani ya masaa manne, licha ya kulimaliza lakini alikumbana na changamoto mbalimbali ikiwemo sindano kuvunjika kwa zaidi ya mara tano. Lakini pia kwakua hakuwa na mdhamini alilipa asilimia 70 ya gharama mwenyewe.
Vazi hilo lilihitaji takriban mita 56.7 za kitambaa cha Jampard takriban mita 1.83 kwa mwili na takriban mita 54.87 kwa mikono ile ya rekodi.
Leave a Reply