Mj Alitumia Mapigo Ya Moyo Kwenye Wimbo Smooth Criminal

Mj Alitumia Mapigo Ya Moyo Kwenye Wimbo Smooth Criminal

Unafahamu kuwa Michael Jackson alitumia mapigo ya moyo kama mdundo kwenye wimbo ‘Smooth Criminal’ uliotoka mwaka 1987 ndani ya albamu ya Bad.

Inaelezwa kuwa kwa msaada wa daktari wake binafsi, Dkt. Eric Chevlen, Michael alipokuwa studio aliunganishwa kifaa maalumu kilichorekodi sauti ya mapigo ya moyo moja kwa moja kutokea kifuani.

Baada ya kurekodi sauti hiyo ilipelekwa kwa mtaalamu wa muziki Christopher Currell, aliyekuwa akifanya kazi katika mfumo wa ‘Synclavier’. Kisha sauti hiyo ikaongezwa kasi kodogo pamoja na kutengenezwa ili iwe safi zaidi.

Matokeo yake yalikuja kuonekana mwanzoni mwa wimbo huo kabla ya muziki kuanza ambapo mashabiki waliweza kusikia sauti ya mapigo ya moyo ya MJ pamoja na pumzi nzito iliyowavutia mashabiki wengi.



Hata hivyo kwa mujibu Michael alitaka mashabiki wake wasisikie tu muziki, bali wahisi uhai wake kupitia wimbo huo. Ambapo kwenye moja ya mahojiano yake aliwahi kueleza kuwa muziki unapaswa kuwa 'hai' na kugusa au kukonga roho, na njia bora ya kuonyesha hilo ilikuwa kuingiza mapigo ya moyo wake mwenyewe ndani ya muziki.

Kupitia wimbo huo wa Smooth Criminal mapigo hayo yanasikika kuanzia sekunde ya 0:00 hadi 0:06 mwanzoni kabisa mwa wimbo, kabla ya maneno “Annie, are you OK?” kuanza kusikika.

Michael Jackson alipoachia wimbo Smooth Criminal mwaka 1988 , wimbo huo uliandika historia mpya katika muziki wa Pop ukishika nafasi ya saba kwenye Billboard Hot 100 Marekani. Nafasi ya 8 kwenye UK Singles Chart Uingereza huku ukiwa ndio wimbo wa MJ uliotumbuizwa sana kwenye tamasha za Michael Jackson, ikiwemo ziara yake ya Bad World Tour na HIStory Tour.

MJ alifariki dunia 25 Juni 2009 akiwa na umri wa miaka 50, nyumbani kwake huko Los Angeles, Marekani. Sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni overdose ya dawa ya usingizi (propofol na benzodiazepines) ambazo alipewa na daktari wake binafsi, Dr. Conrad Murray, ili kumsaidia kupata usingizi.

Ambapo mchanganyiko huo wa dawa ulisababisha mshutuko wa moyo (cardiac arrest) na kupelekea kifo chake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags