Akizungumza na Mwananchi, Yasinta ambaye aliingiza kama Dorlin kwenye Nsyuka amesema kwa upande wake kuwepo kwenye filamu hiyo ilikuwa kama zali.

“Kwanza niweke marekebisho mimi sio ambaye niliingiza kama Nsyuka. Mimi nilicheza kama Dorlin Nsyuka sijajua kwanini mtayarishaji alinichagua mimi lakini naweza kusema kwangu ilikuwa kama zali tuu. Nilikuwa mtu wa mwisho kufika katika kundi ‘Tamba Art Group’ na tayari kulikuwa na akina Dorlin mwingine.
“Kwa hiyo nilipofika mimi nikapewa sini moja kuifanyia majaribio, na mimi nikafanya kwa ukubwa zaidi. Mara baada ya kumaliza nilijikuta nashangiliwa na ukumbi mzima ikimaanisha kwamba nimeitendea haki ndipo nikachaguliwa kuingia katika Nsyuka mazima,”
Aeleza kuhusu kuwekwa benchi baada ya Nsyuka namba mbili
“Baada ya kuonekana kwenye Nsyuka milango ilifunguka nikaanza kupokea madili mbalimbali ikiwemo kucheza kwenye filamu kama Return of Nsyuka, Siwatu, Fungu la Kukosa. Kulikuwa na movie nyingi, japo kwa Nsyuka namba mbili nilipocheza nilikaa benchi kidogo kutokana na kudai pesa kubwa."anasema
Anasema alidai kiasi kikubwa cha pesa kutokana na majanga yaliyompata wakati anaigiza Nsyuka namba moja.
“Kweli nilipewa ile hela niliyoihitaji lakini baada ya filamu kuisha nikawekwa benchi. Nikakaa karibu mwaka mmoja bila kuigiza chochote, lakini baada ya hapo nikarudi tena na movie yangu ya mwisho ikawa ni Sawaka iliyotoka mwaka 2016-17. Baada ya hapo nikapotea mazima kwenye tasnia ya filamu mpaka nakuja kuibuka kwenye Kombolela,”amesema.
Mbali na Nsyuka filamu nyingine alizoigiza za kutisha ni pamoja na Chite Ukae, Sawaka, pamoja na Return of Nsyuka.
Akizungumza kuhusu Kombolela na namna alivyokuta na Abdul
“Kwangu Kombolela ni tamthilia ambayo nitaiheshimu sana katika maisha yangu. Na kaka yangu Abdul hatotoka kwenye moyo wangu ameweka alama kubwa sana kwa sababu hii ndio kazi yangu ya kwanza baada ya muda mrefu. Kwangu imeweka alama kubwa sana angalau imeweza kurudi watu kutambua uwepo wangu.

“ Siku nilikuwa na mdogo wangu Halima Yahya ‘Davina’ kwenye mizunguko yetu akaniomba tupite ofisini kwa Abdul. Baada ya kufika pale likaibuka shangwe lenye vilio ndani yake kumbe Abdul alikuwa akinitafuta siku zote na hakujua pakunipata, akaniambia kesho unatakiwa kuwasili kambini kwa ajili ya kuigiza Kombolela uhusika wa Yasinta,” amesema.
Leave a Reply