Mambo kumi kuhusu Jux

Mambo kumi kuhusu Jux

Jina la Jux limeendelea kujizolea umaarufu katika Bongofleva na kimataifa hasa miaka ya hivi karibuni, muziki na mtindo wake wa maisha kama chapa umemfanya kuwa miongoni mwa wasanii ghali sana kwa sasa.

Akiwa ametoa albamu na kushinda tuzo za ndani na kimataifa, Jux anazidi kukonga nyoyo za mashabiki wake kwa muziki mzuri ambao umepata mamilioni ya wasikilizaji mtandaoni. Fahamu zaidi.

1. Hadi sasa akiwa na miaka zaidi ya 10 katika muziki, Jux ametoa albamu mbili, The Love Album (2019) na King of Hearts (2022), pamoja na Extended Playlist (EP) moja, A Day To Remember (2025) yenye nyimbo saba.

2. Kufuatia kufanya vizuri na wimbo wake, Ololufe Mi (2024) aliomuimbia mkewe Priscilla, Jux ameshinda tuzo za kimataifa kama Trace zilizofanyika Zanzibar akishinda kama Msanii Bora wa Kiume Tanzania 2024. Pia alishinda tuzo ya Headies huko Lagos, Nigeria akinyakua kipengele cha Msanii Bora Afrika Mashariki 2025 akiwabwaga wakali kama Bien (Kenya), Diamond Platnumz (Tanznaia), Bruce Melodie (Rwanda) na Azawi (Uganda).

3. Video ya wimbo wake, Enjoy (2023) ilishatazamwa zaidi ya mara milioni 100 YouTube, hivyo akawa msanii wa nne Tanzania kuwa na video yenye namba hizo baada ya Diamond (Yope Remix, Inama, Waah!, Jeje na Nana), Harmonize (Kwangwaru) na Zuchu (Sukari).

4. Nyimbo za Jux ambazo zimepata namba za juu zaidi katika majukwaa ya kidijitali ya kusikiliza muziki, zote zimetengenezwa na S2kizzy ambaye alianza kutengeneza midundo baada ya kumaliza kidato cha nne huko Mbeya.

5. Tayari Jux amefanya kazi na rapa wa Nigeria, Phyno aliyesikika katika wimbo wake, God Design (2025), akiwa ni msanii wa pili Bongo kushirikiana na Phyno baada ya Rayvanny aliyemshirikisha katika wimbo wake, Slow (2019). Meneja wa WCB Wasafi na Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki aliyemaliza muda wake, Babu Tale, anamtaja Phyno kama rapa wake bora kwa muda wote kutokea ukanda wa Afrika Magharibi.

6. Jux alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) 2023 katika kipengele cha Wimbo Bora wa Kushirikiana (Enjoy) akiwa na Diamond ambaye wameshirikiana katika nyimbo nyingine kama Sugua (2019) na Ololufe Mi (2024).

7. Chino Kidd amecheza katika video ya wimbo wa Jux, DJ Tarico na G Nako, Shugga Daddy (2023), ni kwa sababu hiyo ni kazi yake na aliwahi kushinda tuzo ya TMA kama Dansa Bora wa Mwaka. Na baada ya kuanza kusimama kama mwanamuziki, Chino alishinda TMA kama Msanii Bora Chipukizi 2023 akiwabwaga Xouh, Appy, Mocco Genius na Yammi.

8. Jux ni mwanamuziki wa pili wa Bongofleva kwa wimbo wake (God Design)  kushika namba moja katika chati ya iTunes nchini Nigeria. Wa kwanza kufanya hivyo ni Diamond kupitia wimbo wake, My Bay (2023) akimshirikusha Chike wa Nigeria pia.

9. Mke wa Jux, Priscilla ndiye mrembo aliyetokea kwenye video nyingi zaidi za mwanamuziki huyo zikifikia nne - Ololufe Mi (2024), Si Mimi (2025), God Design (2025) na Thank You (2025) ambayo imetoka baada ya kutangaza kutarajia mtoto.

10. Wakati wanatangaza uhusiano wao mnamo Juni 2024, Priscilla alikuwa na wafuasi milioni 2.8 katika ukurasa wake wa Instagram ila sasa ikiwa ni mwaka mmoja, wamefikia milioni 4.1, hivyo akiwa na staa huyo wa Bongofleva ameongeza wafuasi milioni 1.3.

Hii ina faida kwa Priscilla upande wa kazi yake ya ushawishi wa chapa mtandaoni ambapo amewahi kufanya kazi na kampuni ya cryptocurrency ChiJ14Exchange, kampuni ya utengenezaji wa filamu ya Viskit, chapa ya vipodozi Hegai and Esther.

Narudia tena, naamini Diamond hajawatuma hawa watu lakini nashindwa kujizuia kusema anawaruhusu kwa namna moja au nyingine. Kwa sababu kama kuna mtu anatoa taarifa zako usizopenda zitolewe na wewe humzuii bado unaendelea kuwa naye karibu na bado anaendelea kupata taarifa zako zingine na zingine maana yake ni kwamba umemruhusu bila kumwambia fanya.

Tutumie mfano wa baba na mtoto kwa sababu Baba Levo anamuita Mondi baba yake. Ikiwa mtoto wako anaamka asubuhi anasimama uwanjani na kuanza kutukana majirani halafu wewe baba unakuja kusema hujamtuma, lakini humzuii wala kumuadhibu kiasi kwamba kesho ana uwezo wa kuamka na kutukana tena, hiyo inamaanisha nini?

Diamond alishakuwa mkubwa sana pengine washkaji wa kitaa kama hivi hatuwezi tena kumshauri, lakini bila kujali kama anashaurika au la sisi tutamwambia ukweli. Kama kweli anachukia yanayofanya na chawa wake, basi anatakiwa kuwapunguza au kuwakomesha kusema wanayosema. Sio kila siku wanasema halafu anakuja kutuambia hajawatuma.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags