D Voice Atuma Maombi Haya Kwa Waandaaji Wa Tuzo

D Voice Atuma Maombi Haya Kwa Waandaaji Wa Tuzo

Mwanamuziki wa singeli na Bongo Fleva nchini D Voice amewaomba waandaji wa tuzo za muziki nchini kuongeza vipengele kutokana na muziki wa singeli kukua.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameshare ujumbe akieleza kuwa kutokana na Singeli kukua hivyo basi angeomba kuongezwe baadhi ya vipengele kikiwemo tuzo ya heshima kwa mwanzilishi wa Singeli.


“Kutokana na huu ukuwaji wa muziki wa Singeli tunaomba tuzo ziongezwe, ikiwemo Mwandishi bora wa Singeli, Tuzo ya msanii mpya wa Singeli, Wimbo bora wa kushirikiana wa Singeli, Video bora yam waka ya Singeli pamoja na Tuzo ya heshima ya mwanzilishi wa Singeli ambayo hii ni lazima iende kwa Legend Msaga Sumu,”ameandika D Voice

Aidha kufuatia na ujumbe huo wanamuziki mbalimbali wa Singeli wametoa maoni yao akiwemo Dulla Makabila ambaye amempongeza D Voice kwa wazo hilo alilolitoa.

Hata hivyo haya yanakuja baada ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuweka wazi kuwa ipo katika hatua za mwishoni kuufanya muziki wa singeli kuingia kwenye orodha ya urithi wa dunia.

Hayo yalielezwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Methusela Ntonda, Agosti 19, 2025, jijini Dar es Salaam, alipofungua mkutano wa wadau wa utamaduni walioshiriki kuandaa orodha hiyo.

“Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha orodha ya Kitaifa ya Urithi wa Utamaduni Usioshikika ikiwa ni hatua ya kukamilisha mchakato wa Uteuzi wa Muziki wa Singeli kwenye orodha ya kimataifa ya UNESCO,”alisema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags