Kama umezoea kuacha chakula katika migahawa unayokwenda huku waandaaji na wahudumu wakichukulia jambo la kawaida, lakini hii ni tofauti kwa mgahawa mmoja kutoka Las Angeles, Marekani ambapo mtu huchapwa viboko asipomaliza chakula.
Mgahawa huo unaojulikana kwa jina la ‘Heart Attack Grill’, unatajwa kuwa ndio mgahawa unaotengeneza baga tamu zaidi lakini moja ya sheria ya mgahawa huo ni kuwa licha ya malipo atakayoyafanya mteja basi asipomaliza chakula chake atachapwa viboko na muhudumu mbele ya wateja wengine.
Aidha inaelezwa kuwa viboko hivyo si adhabu bali ni kama burudani yenye utani ndani yake huku ikidaiwa kuwa kama ni onyo kwa wale wapenda kula kupindukia.
Mgahawa huo ulianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 2005 na Jon Basso maarufu kama ‘Doctor Jon’ huku jina la mgahawa huo ‘Heart Attack Grill’ likitolewa kutokana na chakula chao kuwa hatari kwa moyo. Ambapo vyakula vyao vinatajwa kuwa vyenye mafuta na kalori nyingi kiasi cha kuashiria kuwa mtu anaweza kupata heart attack kama atakula mara kwa mara.
Hata hivyo inaelezwa kuwa msemaji wa mgahawa huo Blair River alifariki dunia akiwa na miaka 29 mwkaa 2011 kwa ugonjwa wa moyo huku akiripotiwa kuwa na kilo takribani 500. Mbali na huyo naye mteja aliyekwenda kula mara kwa mara katika mgahawa huo aitwaye John Alleman alifariki dunia kwa shambulio la moyo mwaka 2013.
Jambo la kipekee katika mgahawa wa ‘Heart Attack Grill’ madhari yake ni tofauti na migahawa mingine, ambapo mandhari ya mgahawa huo ipo kama hospitali, wahudumu wanavalia mavazi ya wauguzi (nurses) huku Doctor Jon akionekana kama Daktari mkuu wa mgahawa.
Kwa upande wa wateja wanapokelewa kwa kauli ya utani “Karibu wagonjwa!” ambapo wanahesabiwa kama wagonjwa, wakiingia kwenye hospitali-themed restaurant, huku wakiveshwa mavazi kama wagonjwa. Na ambao wenye kilo kuanzia 160 hula bure.
Baadhi ya watu mashughuli ambao wamewahi kuhudhulia katika mgahawa huo ni pamoja na BeardMeatsFood, Nikocado Avocado, Gabriel "Fluffy" Iglesias, Matt Stonie na wengineo.
Leave a Reply