Chioma alionekana tena Instagram Agosti 21,2025 kwa mara ya kwanza tangu msiba wa mtoto wake wa kwanza, Ifeanyi, aliyefariki dunia mwaka 2022. Katika chapisho hilo Chioma ameshare pete ambayo aliivaa siku ya harusi yake ikionesha picha ya marehemu mwanaye.
Katika chapisho hilo, liliambatana na ujumbe usemao “Rafiki yangu wa karibu ndiye aliyeniongoza kwenye maisha ya milele… Ify, nakuwaza kila siku na unaishi moyoni mwangu. Milele na daima. Kwa upendo, mama,” huku Davido akijibu “Hadi milele”.

Kabla ya posti hiyo chapisho lake la mwisho pia lilikuwa ni picha ya mwanaye aliyoichapisha mwaka 2022 akimtakia kheri katika siku yake ya kuzaliwa.
Mbali na Chioma kuvalia pete yenye picha ya mwanaye, naye mwanamuziki Davido katika siku ya harusi yao iliyofanyika Miami ‘White Wedding’ alionekana akiwa amevalia suti yenye vishikizo ‘Vifungo’ vya picha ya marehemu mwanaye tukio ambalo liliibua hisia tofauti kwa mashabiki duniani kote.
Utakumbuka Ifeany alifariki dunia Oktoba 31, 2022 baada ya kuanguka kwenye bwawa la kuogelea nyumbani kwao, Banana Island, Lagos, Nigeria.
Leave a Reply