Yammi Ajitosa Kwenye Singeli

Yammi Ajitosa Kwenye Singeli

Msemo wa msanii mkongwe wa Singeli Msaga Sumu, kuwa kila msanii wa nyimbo za aina nyingine ipo siku atakuja kuimba Singeli, umeanza kuonekana.

Baada ya wasanii Zuchu, Jux, Diamond Platnumz, Harmonize, Mbosso, Ali Kiba na wengine kuimba Singeli, sasa ni zamu ya Yammi ambaye ameachia wimbo wa singeli leo.

Kupitia Ep yake iliyotoka masaa machache yaliyopita Yammi amejitosa kwenye singeli ukiwa ni wimbo wake wa kwanza wa aina hiyo uitwao ‘Sijafunzwa’ akimshirikisha Mdogo Sajenti.

Ep hiyo iliyopewa jina la ‘After All’ yenye ngoma sita ni kazi yake ya kwanza kubwa kuachia tangu aachane na lebo ya African Princes. Ikumbukwe lebo hiyo iliyomsaini Yammi Januari 20, 2023 na ilitangaza kutemananae mwezi Mei mwaka huu.

Hata hivyo msanii huyo ameachia ngoma moja ambayo ni Raha iliyotoka Juni 6, 2025 ikifanikiwa kutazamwa zaidi ya mara 762,284 katika jukwaa lake la Youtube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags