Mmoja apigwa risasi wakati wa maandamano nchini Kenya

Mmoja apigwa risasi wakati wa maandamano nchini Kenya

Mtu mmoja amepigwa risasi karibu na soko, katika makazi duni ya Kibera katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wakati maandamano yakiendelea katika jiji hilo.

Moja ya chombo cha habari kutoka nchini Kenya kimeripoti kuwa mfanyabiashara huyo alipiga kelele kuwa yeye ni fundi mitambo, wala si muandamanaji.

Mfanyabiashara huyo inasemekana kuwa alipigwa risasi na afisa wa polisi. na amepelekwa hospitalini kwa pikipiki.

Kinara wa upinzani Raila Odinga amepata uungwaji mkono mkubwa katika eneo hilo. Pia ufikiaji wa baadhi ya sehemu jijini humo umekuwa vigumu kwasababu kumewekwa vikwazo ili kuzuia watu kukusanyika.

Hii inakuja baada ya  chama cha upinzani kuitisha maandamano makubwa yaliyopangwa kupinga gharama ya juu ya maisha na kile wanachokiita urais usio halali.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags