Mastaa wamlilia hayati Mzee Mwinyi

Mastaa wamlilia hayati Mzee Mwinyi

Kufuatiwa kutangazwa kwa kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Ali Hassan Mwinyi, mastaa mbalimbali wameoneshwa kuguswa na msiba huo.

Katika kuonesha majonzi yao kila mmoja kwa nafasi yake amechukua wasaa wa ku-share ujumbe wa kuomboleza kupitia kurasa zake za mtandao wa kijamii.

Mastaa hao ni pamoja na Diamond, Mwana-FA, Aslay, Mrisho Mpoto, Dulla Makabila, Ommy Dimpoz, Shilole, Marioo, Lady Jaydee, Nikk wa Pili, Roma, Joti, Peter Msechu, Zuchu, Nandy, Zamaradi na Jux.

Hakika leo umeufunga rasmi ukurasa wa kitabu cha hadithi yako,R.I.P Mzee wetu Mh.Ali Hassan Mwinyi,Rais Mstaafu wa Awamu ya pili, Pole kwa Familia/Ndugu/Jamaa na Marafiki, pamoja na Serikali,” aliandika Joti.

“R.I.P Mzee Ruksa Allaah akupe kauli thabit my condolences to President Dk H Mwinyi and whole family”: Ommy Dimpoz.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi amin”: Diamond.

“Mr Ruksa, uchumi wa soko, uhuru wa mitaji, mawazo na bidhaa ulifungua milango ya sisi kushiriki kwenye uchumi wa soko la dunia. Asante kwa uongozi wako na maisha yako, pumzika salama”: Nikki wa Pili.

Mwinyi alifariki dunia siku ya jana, Februari 29, 2024, majira ya saa 11 jioni katika Hospitali ya Mzena Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, alipokuwa akipatiwa matibabu ya saratani ya mapafu.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags