Maporomoko ya ardhi yauwa watu 11 nchini Cameroon

Maporomoko ya ardhi yauwa watu 11 nchini Cameroon

Maporomoko ya ardhi yameuwa watu wasiopungua 11 waliokuwa kilioni katika mji mkuu wa Cameroon, Yaounde. Maafisa wa eneo hilo wamesema wahanga walikuwa wamekusanyika juu ya kilima katika ibada ya mazishi ya watu watano, wakati ardhi waliyoikalia ilipoporomoka.

Mmoja wa maafisa hao amesema baadhi ya watu wamesombwa pamoja na hema walimokuwa wamekaa. Shughuli za uokozi ziliendelea hadi giza lilipoingia jioni ya jana na zitaanza upya leo asubuhi.

Mmoja wa mashuhuda amesema watu walikuwa wameanza kucheza ngoma za maombolezo wakati ardhi chini ya miguu yao ilipoanza kuporomoka.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags