Mahakamani kwa kuwavunjia heshima Rais Samia na Kikwete mtandaoni

Mahakamani kwa kuwavunjia heshima Rais Samia na Kikwete mtandaoni

Piniston Nzali (20) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam akidaiwa kuchapisha mtandaoni taarifa zenye kuharibu hadhi ya Rais Samia Suluhu na Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Imeelezwa, kupitia mtandao wa TikTok, mtuhumiwa alichapisha picha mjongeo (video) zinazoonesha viongozi hao wakiimba jambo ambalo halikuwa na uhalisia.

Aidha, tuhuma nyingine ni kutumia laini ya simu inayomilikiwa na mtu mwingine bila kutoa taarifa ya mabadiliko ya umiliki kwa mtoa huduma. Mtuhumiwa amekana tuhuma zote.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags