Kenya yaweka agizo la kuwa na sehemu moja ya starehe kila mji

Kenya yaweka agizo la kuwa na sehemu moja ya starehe kila mji

Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua ametoa amri kwa viongozi wa serikali za mitaa nchini humo kutekeleza agizo la kuwa na sehemu ya starehe (bar) moja kwa kila mji.

Rigathi Gachagua pia anataka maeneo ya burudani katika eneo hili kufanya kazi kati ya saa kumi na moja hadi saa tano usiku katika hatua mpya zinazokusudiwa kukabiliana na ulevi.

Kuna hofu kwamba maagizo yanaweza kuwafanya watu wengi kutumia pombe za kujitengenezea nyumbani ambazo zinawekwa kemikali za viwandani.

Vifo vilivyotokana na pombe haramu vimeripotiwa hapo awali.

Lakini Gachagua alisema siku ya Alhamisi kuwa ulevi katika eneo hilo ni mbaya na akawaambia maafisa wasisajili upya leseni zao za maeneo ya starehe zitakapoisha.

“Haya mambo tuyashughulikie, tuokoe kizazi kijacho vinginevyo tutakuwa na matatizo katika jamii yetu,” alisema Naibu Gachagua.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags