Ebwanaa, hivi umeshawahi kuhisi ama kujiuliza kama kuinua vitu vizito zaidi huuenda ikawa sababu ya kuongeza uwezo wa kuishi muda mrefu zaidi duniani?
Haya bwana sio maneno yangu ila ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Dk Jessica Gorzelitz.
“Utafiti wetu umebaini kuwa hatari ya kifo ilipungua zaidi miongoni mwa wale walioshiriki katika mazoezi mepesi na yale ya kuimarisha misuli," alisema mwandishi wa utafiti huu Dk Jessica Gorzelitz.
Kidogo kinajulikana kuhusu athari za kunyanyua uzani au mazoezi ya kuimarisha misuli juu ya muda gani watu wanaishi.
Lakini utafiti mpya umesema kuwa inaweza kuwa ufunguo wa maisha marefu.
Watafiti wa Marekani wamegundua kuwa shughuli zinazoimarisha misuli - kama vile kunyanyua vitu vizito - zinapaswa kuwa sehemu ya mazoezi ya kila wiki pamoja na mazoezi ya mepesi au (aerobics) kama vile kukimbia na kuogelea.
Lakini sio lazima tu kwenda kwenye ukumbi wa mazoezi ili kutunisha misuli … unaweza kubeba mifuko mizito, kufanya kazi ngumu au kutembea Kwa haraka au kulima shambani, vyote ni muhimu maathalani ukiwa na umri uliozidi miaka 65.
Wizara ya afya Marekani inawashauri watu wazima walio na umri wa zaidi ya miaka 65 kuwa na mazoezi ya viungo kila siku. Pia wanahitajika kufanya shughuli za kuimarisha nguvu na mazoezi mepesi angalau mara mbili kwa wiki.
Kiafrika tunafunzwa kuwasaidia wazee wetu kubeba mizigo “wasije wakaumiza migongo.”
Aloooh sasa itakuaje jaman na hizi tafiti. Haya, dondosha maoni yako hapo chini kuhusiana na utafiti huo.
Chanzo BBC
Leave a Reply