Helikopta yaua watu 22 Congo

Helikopta yaua watu 22 Congo

Takribani watu 22 wameuwawa wakati helikopta mbili za jeshi la Uganda zilipoanguka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa hizo zimetolewa na msemaji wa jeshi la Congo ambaye hakutaka kutajwa majina wakati alipozungumza na shirika la habari la Reuters hivi leo.

Aidha, msemaji huyo pia amedokeza kuwa jeshi la Uganda bado mpaka sasa halijawafahamisha kuhusu mazingira ya kuanguka kwa helikopta hizo, lakini hakutoa maelezo zaidi. Msemaji wa jeshi la Uganda Felix Kulayigye amethibitisha helikopta moja ilianguka na kusema kulitokea vifo, lakini hakuwa na maelezo zaidi kwa sasa.

Uganda ilituma majeshi katika nchi jirani ya Congo mnamo Desemba mwaka uliopita kusaidia kupambana na kundi la waasi la Allied Democratic Forces ADF.

Chanzo DW






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags