Ikiwa leo ni siku ya kumbukizi ya kuzaliwa ya mwanamuziki Marioo, mzazi mwezie na mfanyabiashara Paula Kajala amempatia maua yake mpenzi wake huyo huku akiweka wazi kuwa amefanikiwa katika maisha kwa sababu ya Marioo.
“Heri ya kuzaliwa mpenzi wangu, rafiki yangu wa karibu, mshirika wangu, na baba wa watoto wangu. Unapoanza mwaka huu mpya, nataka ujue kwamba wewe ni baba bora sana kwa mtoto wetu. Ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kushiriki safari hii nzuri ya ulezi pamoja nawe. Umekuwa mtu wa maana sana katika maisha yetu, na ninaweza kusema kwa uhakika kwamba nimefanikiwa sana maishani kwa sababu yako.
Neema ya Bwana iwe juu yako daima. Mungu akubariki katika kila unachokifanya, kikafanikiwe, na uendelee kuwa bora zaidi kila siku. Wewe ni kila kitu kwangu, NA NAKUPENDA SANA,” ameandika Paula
Uhusiano wa wawili hao ulianza kushamiri katika mitandao ya kijamii mwanzoni mwa mwaka 2023 ambapo mpaka kufikia sasa Marioo na Paula wamefanikiwa kupata mtoto wa kike aitwaye Amarah.
Leave a Reply