Zuchu Ashika Namba Moja Zimbabwe

Zuchu Ashika Namba Moja Zimbabwe

Mwanamuziki anayetamba na Album yake ya ‘Peace and Money’ Zuchu ameripotiwa kushika namba moja nchini Zimbabwe kupitia wimbo wake wa Kwikwi.


Kupitia tovuti ya iCharts imeshare orodha ya ngoma ambazo zimesikilizwa zaidi katika mtandao wa iTunes ambapo msanii Zuchu ameibuka namba moja kupitia ngoma yake hiyo aliyoiachia miaka miwili iliyopita.



Wasanii wengine ambao ngoma zao zimeingia katika orodha hiyo ni pamoja na Kendrick Lamar, Dr Dre, Tyler ICU, Kari Jobe na wengineo.


Mpaka kufikia sasa wimbo huo wa Kwikwi umesikilizwa zaidi ya mara milioni 63 katika mtandao wa YouTube.

Kwa Sasa msanii huyo anatamba na albumu yake ya kwanza iitwayo ‘Peace and Money’ akiwashirikisha wasanii kama Diamond, Yemi Alade, Spyro, D Voice na wengineo huku album hiyo ikiwa na ngoma 13.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags