Angelina Jolie Na Brad Pitt Watalikiana Rasmi

Angelina Jolie Na Brad Pitt Watalikiana Rasmi

Baada ya kuburuzana mahakamani kwa takribani miaka nane kufuatia na madai ya talaka, hatimaye mwigizaji Angelina Jolie na aliekuwa mumewake Brad Pitt wamepeana talaka rasmi.

Taarifa hiyo imetolewa na wakili wa Jolie, James Simon, wakati alipokuwa kwenye mahijiano na jarida la People ambapo amedai kuwa talaka hiyo imetoka rasmi jana Jumatatu Desemba 30, 2024.

“Hii ni sehemu moja tu ya mchakato mrefu unaoendelea ambao ulianza miaka minane iliyopita, Kusema ukweli Angelina amechoka lakini amefarijika sehemu hii moja imekwisha,” amesema James Simon

Jolie aliwasilisha kesi ya talaka Septemba 2016, ambapo kesi hiyo ilifuatiliwa kwa ukaribu mpaka mwaka 2018 na mahakama iliwaruhusu kufikia makubaliano ya malenzi ya watoto wao sita pamoja na mgawanyo wa mali lakini suala hilo lilikuwa gumu kwa wawili hao na kupelekea kuingia kwenye mzozo wa muda mrefu.

Jolie mwenye umri wa miaka 49 na Pitt mwenye umri wa miaka 61 walikuwa ni wanandoa maarufu Hollywood kwa zaidi ya miaka 12 ambapo ndoa hiyo ilikuwa ya pili kwa Pitt, kwani hapo awali alifunga ndoa na nyota wa Friends, Jennifer Aniston na kwa upande wa Jolie ilikuwa ndoa ya tatu baada ya kuolewa na waigizaji Billy Bob Thornton na Jonny Lee Miller.


Wawili hao wameonekana katika filamu ya pamoja kama Mr. & Mrs. Smith, By the Sea, Atlas Shrugged na nyinginezeo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags