Albamu maarufu ya SZA inayofahamika kama SOS imerudi tena kwa kishindo ambapo imeshika nafasi ya kwanza katika chati ya Billboard 200, ikiwa ni miaka miwili tangu kuachiwa kwake.
Kuibuka upya katika chati hizo ni baada ya SZA kuachia toleo la pili la albumu hiyo iitwayo Deluxe iliyoachiwa Desemba 20 inayofahamika kama SOS Deluxe: LANA, ambapo ameongeza nyimbo 15 mpya ukiachana 23 za mwanzo.
Matoleo yote mawili ya albamu hiyo yalipata mauzo ya 178,000 nchini Marekani katika wiki iliyoishia Desemba 26, ikionesha ongezeko la asilimia 297 kwa mujibu wa ripoti ya Luminate.
Hii inaifanya album hiyo kuongoza chati kwa wiki 11, mafanikio ambayo mara ya mwisho aliyapata Machi 2023.
Leave a Reply