Mawakili wa utetezi wa Diddy wametoa hati mpya Mahakamani ya kupinga madai ya kuwa video zinazomuhusu rapa huyo na aliyekuwa mpenzi wake Cassie Ventura kuwa zilirekodiwa kwa kificho.
Hati hiyo iliyofikishwa mahakamani jana Jumanne Januari 14, 2025 imeeleza kuwa kwenye video tisa ambazo zimepatikana nyumbani kwa Diddy waendesha mashitaka wanaamini rapa huyo alidhamiria kurekodi huku mawakili wa Combs, Marc Agnifilo na Teny Geragos wakiomba kupatiwa video hizo wazitazame tena kwa makini kwani wanaamini tukio hili lilikuwa ni la hiari.
Aidha mawakili hao wamedai kuwa walichokiona katika video hizo ni matukio ambayo yalikuwa ya kibinafsi kati ya watu wazima waliyokubaliana kwa muda mrefu licha ya serikali na mahakama kuiaminisha vibaya jamii.
“Video hizi bila shaka zinaonyesha kwamba mtu anayedaiwa kwenye hati ya mashtaka kuwa ‘victim 1’ si tu alikubali bali alifurahia kwa kina.
Katika msingi wake, kesi hii inahusu kama victim-1 alikuwa au si mshiriki mwema wa maisha yake ya ngono binafsi na Bwana Combs. Video hizi zinathibitisha wazi kwamba alikuwa hiari,” wamesema Marc Agnifilo na Teny Geragos
Leave a Reply