Katika Kijiji Hichi Kila Mtu Hutungiwa Wimbo Kama Jina La Utani

Katika Kijiji Hichi Kila Mtu Hutungiwa Wimbo Kama Jina La Utani

Kwa kawaida tumezoea kuona kuwa wasanii hutunga na kutoa wimbo kwa ajili ya kufurahisha na kuburudisha jamii, lakini hii ni tofauti kutoka katika kijiji kilichopo Meghalaya Kongthong Kaskazini-Mashariki mwa India maarufu ‘Whistling Village’ ambapo watu wengi hutungiwa wimbo kama jina la utani.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali utamaduni huo ulianza karne nyingi ambapo mtoto anapokuwa tumboni kwa mama yake, basi mama huyo anaanza kumuimbia wimbo ili aanze kuukalili, kuusikia na pindi atakapo zaliwa wimbo huo usiwe mgeni masikioni kwake.

Jina hilo ambalo ni wimbo wa sekunde 14-18 unakuwa kitambulisho cha mtu husika kwa maisha yake yote na mara mtu atakapofariki, wimbo wake hupotea na huwa haurudiwi kwa kupewa mtu mwingine kamwe.

Aidha lengo kubwa ni kila mmoja wapo kuwa na jina la kipekee ambalo ni la utani, lakini pia jina hilo hutumika hasa watu wanapokuwa mashambani na kwenye uwindaji ambapo ulitumia kumuita mtu aliye mbali.

Mbali na hilo lakini wakazi wa kijiji hicho wanaamini kuwa kumuita mtu msituni kwa jina lake sio vizuri kwani roho chafu zinazurura misituni hivyo kumuita mtu kwa melodi au wimbo roho hizo hazitambui majina hayo kwa undani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags