Kanye West Hana Mpinzani Kwenye Biashara

Kanye West Hana Mpinzani Kwenye Biashara

Rapa kutoka Marekani Kanye West ameonesha ukubwa wake kwenye biashara, hii ni baada ya kuripotiwa kupata mauzo ya dola milioni tatu kupitia bidhaa zake za YZY ndani ya masaa 30.

Mauzo haya yalitokana na uzinduzi wa hivi karibuni wa bidhaa na mitindo mipya ya Yeezy, ambayo ilitoa mavazi na viatu vya toleo maalum na la kipekee.

Tangazo la uzinduzi huo lilipostiwa kupitia mitandao rasmi ya kijamii ya msanii huyo na kupokelewa kwa ukumbwa na mashabiki huku mkusanyiko huo ukiongeza mapato na utajiri zaidi wa msanii huyo.

Kama mtu mashuhuri katika muziki na mitindo, hii ni mojawapo ya nyakati nyingi ambazo West ameonesha uwezo wake wa kufanikisha mafanikio makubwa ya kibiashara hata mwanzoni mwa mwaka ambapo uchimi unakuwa haujakaa sawa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags