Tumzingatie Rapcha ana kitu chake kwenye Muziki

Tumzingatie Rapcha ana kitu chake kwenye Muziki

Gemu ya Hip-hop Tanzania kwa sasa ina majina mengi ya wasanii wanaofanya vizuri hususani wa kizazi kipya ambao kwa pamoja wanaitwa 'New Generation Ya Rap' hapo utakutana na kina Rapcha, Boshoo, Maarifa, Young Lunya, Country Wizzy, Moni Centrozone, Msamiati, na wengine wengi.

Rapcha ni miongoni mwa wasanii wa Hip-hop wa New Generation ambaye kabla ya kuanza kujitegemea kimuziki 2025 alikuwa chini ya lebo ya Bongo Records ambayo inamilikiwa na mtayarishaji nguli wa muziki wa Hip-hop nchini 'P Funky' Majani, ambapo amekuwa akifanya kazi na lebo hiyo tangu aliposainiwa mwaka 2019.

Rapcha ni pakeji ya vitu vingi ndani ya msanii mmoja akiwa na uwezo wa kuimba au kurap kwa usimuliaji, kuimba Bongo Fleva, na kunata kwenye biti ngumu za Hip-hop kitu ambacho kinamuweka msanii huyo kwenye nafasi kubwa ya kusikilizwa na mashabiki wengi wa muziki wake huku akipokea sifa nyingi kutoka kwa wakali wa gemu wakimtaja kama miongoni mwa waandishi wakali sana wa Hip-hop kwa sasa.

Uwezo wake wa uandishi wa usimuliaji, Rapcha amekuwa miongoni mwa wasanii wachache wa muziki wa Hip-hop ambao wanaweza kuweka ujumbe wao kwa njia ya simulizi na watu wakaelewa kile alichokusudia.

Juni 7, 2021 Rapcha aliachia ngoma ya Lissa, moja kati ya nyimbo za Hip-hop zenye simulizi ndani yake iliyopokelewa vizuri sana, tunaweza kusema ndio ngoma iliyomtambulisha kwenye ramani ya muziki kwa kiasi kikubwa sana kwa kumuweka kwenye nafasi nzuri ambapo mashabiki wengi waliamini uwezo wake. Ngoma hiyo imefanikiwa kutazamwa zaidi ya mara milioni 2.3 Youtube.

Rapcha hakuishia kwenye ngoma ya Lissa pekee kufanya rap ya mtindo wa simulizi na mashabiki wakaitika, ameendelea kuonesha uwezo wake huo kupitia nyimbo zake nyingine kama vile Interview, Fungua, Israel & Palestine Tears Ft Viisugar Boy na nyingine nyingi ambapo mpaka sasa anaingia kwenye orodha ya miongoni mwa Rapa wenye uwezo wa kuweka ujumbe na ukaeleweka kwa njia ya simulizi kitu ambacho kitambo wakongwe walizoe kukiona kwa msanii kama Professor Jay, hivi karibuni Dizasta Vinna, P Mawenge na wasanii wengine wengi.

Uwezo wa kutengeneza 'verse' kali,
Mashabiki wa muziki wa Hip-hop wamempa hiyo Krauni Rapcha akitajwa kama mmoja wa wasanii noma na mwenye uwezo kunata kwenye biti ngumu za Hip-hop na kutoa verse kali zaidi.

Disemba 25, 2023, Rapcha alikuwa miongoni mwa wasanii wa Hip-hop walioshirikishwa kwenye ngoma ya Merry Christmass ya kwake Izzo Bizzness huku ngoma hiyo ikiwa na rapa wakali zaidi kama Nikki Mbishi, Fredrick Mulla, Orbit Makaveli, Fivara, Frida Aman, Rasco Sembo na Chemical lakini bado mashabiki wengi walichagua verse ya Rapcha na kuitaja kama miongoni mwa verse kali kwenye ngoma hiyo.

Ngoma ambazo Rapcha amezitendea haki kwa kuchora verse kali zaidi ni pamoja na Mula aliyoshirikishwa na Mapanch 'BMB', Amen aliomshirikisha Lady JayDee, Tunashine na nyingine nyingi.

Uwezo wa kuimba
Ukiachana na uwezo mkubwa alionao Rapcha kwenye kuchana pia amekuwa vizuri zaidi anapoamua kutoa nyimbo na kuimba kawaida yaani Bongofleva na R&B, Februari 2, 2023 aliachia ngoma ya 'Ulivyo' ambayo ameimba mwanzo mwisho. Ngoma nyingine ambazo ameimba ni kama vile, Low ambayo mpaka sasa video yake imetazamwa mara 104,000 youtube, Wait na nyingine nying






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags