Jaiva: Sifanyi Shoo Chini Ya Milioni 50

Jaiva: Sifanyi Shoo Chini Ya Milioni 50

Hit Maker wa 'Kautaka', Jaivah ameweka wazi kuwa, kutokana na thamani yake kupanda kwa sasa hafanyi shoo chini ya shilingi milioni 50 lakini itategemea na mazungumzo na makubaliano.

Jaiva ameyasema hayo kupitia mahojiano aliyoyafanya jana Januari 14, 2025 kwenye kipindi cha The Throne ya Crown Media, na kueleza kuwa kutokana na thamani yake kupanda kwa sasa anapokea shilingi milioni 50 kwa ajili ya shoo lakini pia mazungumzo yapo.

"Sitaki kutisha watu ila kwa sasa hivi napokea milioni 50 kwaajili ya shoo ingawa pia unaweza kupiga simu tukazungumza," amesema Jaiva.

Jaiva amezungumzia mafanikio yaliyotokana na ngoma yake ya 'Kautaka' kupokelewa vizuri Kimataifa mpaka kufikia kuchezwa na wasanii wakubwa Afrika akiwemo Davido, Tiwa Savege, Burnaboy, Mr Flavor na wengine wengi.

Hata hivyo suala la wasanii wa Tanzania kujiwekea viwango fulani vya malipo kwenye kazi zao hususani shoo ambazo wamekuwa wakifanya, hazijaanza leo, mwaka 2012 msanii Diamond Platnumz alitangaza kutofanya shoo chini ya shilingi milioni 10, na kuelezea kuwa pesa hiyo inahitajika kugawanywa kwenye timu anayokuwa nayo wakiwemo madansa na wapiga picha.

Japo kwa kipindi hicho zilionekana ni pesa nyingi sana ukilinganisha na kazi ya muziki ilivyokuwa ikichukuliwa na hata wadau mbalimbali wa muziki walimjia juu mpaka kufikia kutopanda kwenye baadhi ya majukwa na kuingia migogoro na watayarishaji lakini kadri miaka ilivyozidi kwenda kiwanda kizima cha burudani kilielewa dhumuni na lengo la msanii huyo baada ya kuleta mapinduzi makubwa kwenye tasnia ya muziki Tanzania.

Lakini pia suala hilo halijaishia tu kwenye sanaa ya muziki pekee bali hata tasnia ya uchekeshaji imefika, utakumbuka mwaka 2023 mchekeshaji Jol Master aliweka wazi hafanyi shoo chini ya shilingi milioni 10 ikiwa ni kiwango cha chini cha malipo ambayo waandaaji wa matamasha ya komedi wanapaswa kumlipa endapo watahitaji huduma yake.

Kiwango fulani cha malipo kwa msanii au mtu yeyote anayefanya kazi au kutoa huduma fulani inaruhusiwa lakini kwa kuzingatia thamani yako au bidhaa yako na kiwango husika ulichoweka.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags