Vanessa Mdee afunguka Muziki wa kidunia Ushetani Mwingi

Vanessa Mdee afunguka Muziki wa kidunia Ushetani Mwingi

Aliyekuwa msanii wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee, ameweka wazi kutorudia kufanya muziki wa kidunia huku akiuhusisha na masuala ya kishetani.

Vanessa ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano na Clouds Media, na kuweka wazi kipindi anajitafuta aliambiwa kazi zake kabla ya kutoka lazima zipite kwa waganga.

"Industry ya muziki ina changamoto ya ushetani, watu wanaamini kwenye miungu zaidi, watu wanatumia sana maagano ya miungu, kuna kipindi nilikuwa natafuta management mpya na huyo meneja niliyempata aliniambia kabla muziki wowote haujatoka lazima waupeleka kwa waganga, nikamuuliza kwani humuamini Mungu akajibu Mungu tunamuamini lakini huu ni utamaduni wetu," amesema Vanessa Mdee.

Wakati akizungumza hayo, pia alisisitiza kuwa hana mpango wa kurudi kwenye muziki wa kidunia.

"Kiukweli mimi sidhani kama nitarudi kwenye tasnia ya muziki wa kidunia, sifikirii kabisa kurudi, hilo ndio jibu. Kwenye upande wa muziki wa injili ni wito unaweza ukatumbukia huko hususani sisi ambao tumeshafanya muziki wa duniani.

"Unaweza kuingia huko na ukatumika kwa lengo ambalo halimpendezi Mungu na mimi sitaki kwenda upande huo kwahiyo Mungu akinifungulia naweza kufanya kwa sababu napenda sana kufanya muziki, napenda kutunga na kuimba lakini kwa upande wa muziki wa injili lazima nipate wito," amesema.

Vanessa kwa sasa yupo nchini Marekani akiwa ameanzisha maisha mapya baada ya kusimama kufanya muziki ambapo miaka mitano iliyopita aliachia Moyo na Bado ft Rayvanny zikiwa miongoni mwa kazi zake za mwishoni kuwabariki mashabiki.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags