Filamu zilizotafutwa zaidi Google 2024

Filamu zilizotafutwa zaidi Google 2024

2024 tunaweza kusema umekuwa mwaka wa uzinduzi na mafanikio katika kiwanda cha filamu duniani hii ni kutokana na filamu nyingi maarufu kuachiwa kama ile ya Deadpool & Wolverine, Moana 2 na Inside Out 2 ya Pixar.

Kutokana na hilo, mtandao wa Google umeachia filamu zinazoongoza kwa kutafutwa zaidi kwenye mtandao huo kwa mwaka 2024, huku nyingine zikiwa hazijaachiwa mwaka huu.

1. Inside Out 2

Inside Out 2 iliyotoka 2024 ni sehemu ya pili ya filamu maarufu ya Inside Out iliyoachiwa mwaka 2015. Filamu hii imezalishwa na Pixar Animation Studios.

Sehemu hii ya pili ya Inside Out iliongozwa na Kelsey Mann na kuzalishwa na Mark Nielsen, huku script ikiwa imeandikwa na Meg LeFauve na Dave Holstein.

Kati ya waigizaji wake ni Amy Poehler, Phyllis Smith, Lewis Black, Diane Lane, na Kyle MacLachlan.

2. Beetlejuice Beetlejuice
Ni filamu iliyoachiwa 2024 iliyoongozwa na Tim Burton na kuandikwa na Alfred Gough na Miles Millar. Filamu hiyo imechezwa na nyota kama vile Michael Keaton, Winona Ryder, Catherine O'HaraJustin Theroux, Monica Bellucci, Jenna Ortega, na Willem Dafoe.

3. It Ends with Us
Ni filamu ya kimapenzi kutoka Marekani ilitolewa 2024, ikiongozwa na Justin Baldoni na kuandikwa na Christy Hall, ilitokana na riwaya ya 2016 ya Colleen Hoover. Filamu hii ndani yake wamecheza nyota kama vile Blake Lively, Baldoni, Brandon Sklenar, Jenny Slate, na Hasan Minhaj.

It Ends with Us ilionyeshwa kwa mara ya kwanza duniani katika ukumbi wa AMC Lincoln Square mjini New York Agosti 6, 2024, na kuachiliwa na Sony Pictures Releasing Agosti 9, 2024. Filamu hii ilikumbana na changamoto za kukosolewa, lakini ilifanikiwa kwenye mauzo ya kifedha, ikikusanya dola milioni 350 duniani kote ikizidi mara dufu bajeti ya kuzalishwa kwake iliyokuwa dola milioni 25.

4.Saltburn
Nafasi ya nne imeshikwa na Saltburn filamu iliyoachiwa mwaka 2023, iliyoandikwa, kuongozwa, na kuzalishwa na Emerald Fennell, ikiwa na waigizaji kama Barry Keoghan, Jacob Elordi, Rosamund Pike, Richard E. Grant, Alison Oliver, Archie Madekwe, na Carey Mulligan.

Filamu iliyoshika namba yani ni Dune: Part Two, zikifuatia Twisters, Deadpool & Wolverine, Despicable Me 4, Terrifier 3 na namba kumi ni Alien: Romulus






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags