Mtayarishaji wa muziki nchini S2kizzy ameweka wazi juu ya uwepo wa kazi na Malkia wa Muziki wa Taarab Khadija Kopa.
Zombie amechapisha video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwauliza mashabiki waanze na kazi ipi kati ya EP au Album na malkia huyo.
"Vipi tuachie kipi eti? Album ya pamoja au Ep ya pamoja," S2kizzy.
Utakumbuka Septemba 16,2024 S2kizzy alionesha nia ya kufanya kazi na Malkia huyo baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram "i Wish A session With The queen Khadija Kopa Zuchu fanya mpango basi,"
Kwa upande wa S2kizzy hatujawahi kutayarisha ngoma za mtindo wa taarabu lakini kwa Khadija tayari amewahi kushirikiana na wasanii wa kizazi kipya na kufanya kazi kwa pamoja kama Diamond Platnumz walipokutana kwenye Nasemanawe 2015, Aslay Usitie Doa 2017, Bright ngoma inaitwa Ndoa humo ndani yupo Bi Khadija Kopa, mzee Juma kakere na Malkia Karen.
Lakini pia miaka minne iliyopita Malkia Khadija alishiriki kwenye kuanzisha safari ya binti yake Zuchu baada ya kufanya naye ngoma ya Mauzauza inayopatikana kwenye Ep ya "IamZuchu" iliyotoka 2020.
Emagine hiyo Combo ya Zombie na Malkia wa Tarabu Bi Khadija Kopa?
Leave a Reply