Baada ya mwanamuziki kutoka Marekani Usher, kuwa mshauri wa muda mrefu kwa msanii Justin Bieber na kuzindua kipaji alichonacho kwa jamii, sasa imeripotiwa kuwa wawili hao huwenda wakawa sio marafiki tena.
Kupitia ukurasa wa Instagram wa Beiber ameonesha kufuta urafiki (unfollow) na Usher licha ya msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma ya ‘Yeah’ kuendelea kumfollow.
Hatua hiyo imewashitua watu wengi wakihoji chanzo cha msanii huyo kufuta urafiki na mshauri wake wa muda mrefu ambaye alimtoa katika tasnia ya muziki huku wengi wao wakihuisha suala hilo na kesi zinazomkabili Diddy Combs.
Ikumbukwe kuwa, Bieber akiwa na umri wa miaka 13 Usher alimtambulisha kwa mkali wa hip hop Marekani Diddy ambaye kwa sasa yupo gerezani kufuatiwa na kesi zinazomkabili za unyanyasaji wa kingono.
Wakati wa ushirikiano wao kwenye muziki wawili hao walifanikiwa kutoa ngoma ya pamoja iliyofanya vizuri ndani na nje ya Marekani iitwayo ‘Somebody to Love’
Leave a Reply