Snura adai anaweza asifike Peponi

Snura adai anaweza asifike Peponi

Licha ya kwamba kwa sasa ameishika dini vilivyo, aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya hususani singeli na filamu, Snura Mushi amewaomba watu wamuombee ili aweze kufika peponi.

Akizungumza na Mwananchi, Snura alisema anaweza kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha watu waache dhambi na kuyafuata anayopenda Mungu, lakini asifike peponi kama watu wanavyotarajia.

“Unajua japo mimi natumia muda mwingi sana kwenye kurasa zangu za kijamii kuwahamasisha watu waache mabaya lakini wanaweza kuingia peponi wasinione hivyo nawaomba sana waniombee na mimi niweze kuuona ufalme wa Mungu nawaomba sana,” alisema Snura.

Julai 2024 Snura alitangaza kuacha muziki rasmi na akaomba nyimbo zake zisipigwe tena. Snura Mushi alitangaza kuacha rasmi muziki na shughuli za kisanaa na kujikita zaidi kwenye dini.

Alizitaka media na watu binafsi kuacha mara moja kufanya hivyo kwa kuwa amebadilisha aina ya maisha yake kabisa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags