Hatimaye msanii maarufu wa uigizaji, Joyce Mbaga (32) maarufu ‘Nicole Berry’ na mwenzake Rehema Mahanyu (31), wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, wameachiwa kwa dhamana.
Msanii huyo na mwenzake walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kivukoni inayoketi Kinondoni, Jumatatu Machi 10, 2025, wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, kutokana na kupokea amana (fedha) kutoka kwa umma bila kibali cha Benki Kuu (BoT).
Msanii huyo na mwenzake wameachiwa leo Jumatatu, Machi 17, 2025, na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Ramadhani Rugemarila, anayesikiliza kesi hiyo, baada ya kutimiza masharti haya ya dhamana.
Nicole amedhamiwa kwa hati ya nyumba yenye thamani ya Sh100 milioni iliyotolewa na mmoja wa mdhamini wake, ambao hata hivyo majina yao hayajafahamika.
Mwenzake, Rehema kwa upande wake amedhaminiwa na Ramadhan Juma pamoja na Joyce Isdon, pamoja na hati ya nyumba yenye thamani ya Sh57 milioni.

Leave a Reply